1. Leibniz-Zentrum Moderner Orient
  2. Events
  3. Outline of Activism of Promoting Kiswahili on a Syntagmatic and Paradigmatic Level
Events
Lecture

Outline of Activism of Promoting Kiswahili on a Syntagmatic and Paradigmatic Level

Swahili Baraza with Aldin Mutembei (University of Dar es Salaam)

Ndugu waheshimiwa, wapendwa wanafunzi na marafiki zetu,

Baada ya muhula wa huku kuanza ni furaha yetu kubwa kutangaza kikao kifuatacho cha Baraza letu la Kiswahili la Berlin (BALAKI-BE) ambacho kitakuwa na mada ifuatayo: Vidokezo vya Harakati za Ukuzaji wa Lugha ya Kiswahili Kisilisila na Kiwima

Aldin Mutembei

Katika wasilisho hili, Aldin Mutembei atayajadili masuala yanayolingana na harakati za ukuzaji wa lugha ya Kiswahili kisilisila na kiwima. Atagusia mjadala mgumu wa Mswahili ni nani maana katika harakati hizi kunajitokeza mawazo kama Kiswahili bora, Kiswahili Fasaha na Kiswahili Sanifu ambayo yanaonyesha kuwa mvutano unaopatikana kati ya Kiswahili-Kiarabu na Kiswahili-Kibantu bado upo. Vilevile atatathmini harakati za kufundisha na kujifunza Kiswahili kwa kutumia lugha nyingine za Kiafrika hapo akiangalia dhana ya Kiafrika katika kuelekea ukomavu wa Kiswahili.

Profesa Aldin Kaizilege Mutembei ni Mgoda wa Kigoda cha Uprofesa cha Mwalimu Julius Nyerere cha Kiswahili cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) ya chuo hicho alipoanzisha na kukamilisha miradi mingi ya utafiti na ya ukuzaji wa Kiswahili barani Afrika na ulimwenguni kote. Vilevile ni Naibu Mkurugenzi wa Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU). Aidha, ni mjumbe wa bodi za uhariri wa majarida kadhaa ya kitaaluma ndani na nje ya Afrika, mwalimu na mtafiti wa fasihi ya Kiswahili na mwandishi wa kazi za kubuni.

Kikao kitafanyika siku ya Jumatatu, tarehe 8 Mei 2023, saa kumi kamili za Ulaya ya Kati (saa kumi na moja za Afrika Mashariki) hapa Taasisi ya Taaluma za Asia na Afrika (IAAW), Chuo Kikuu cha Humboldt Berlin, Invalidenstraße 118, ghorofa ya tatu, chumba na. 315, na vilevile kwa kupitia njia ya Zoom: https://tinyurl.com/2t6fkj4k 

KARIBUNI NYOTE! 

Tafadhalini wajulisheni wapenzi wote wa Kiswahili na marafiki wengine!

Wasalaam,
Kai Kresse, Lutz Diegner na Maxwell Omondi Ondieki

Kama kuna maswali yoyote kuhusu baraza hili tafadhalini mwandikieni mwenzetu: MaxwellOmondi.Ondieki(at)zmo.de

This event is part of the lecture series:
Presentation and Discussion Sessions in Swahili 2023
Baraza la Kiswahili la Berlin

Details