How a Female Author’s Creativity Captured Society’s Attention
KUBWAKU NA KURAMBAA: JINSI UMAHIRI WA MTUNZI WA KIKE ULIVYOTINGISHA JAMII
Tukiongozwa na Stefanie Kolbusa, tutapata undani wa simulizi ifuatayo;
Katika miaka ya 1980-1997 baadhi ya nyimbo za taarab zilitingisha Afrika Mashariki. Hasa nyimbo za taarab zilizoimbwa na mwimbaji maarufu Malika zilivuma sana. Hizo nyimbo zilitungwa na mtunzi Khulaita Muhashamy, mzaliwa wa Mombasa.
Kinyume na watunzi wa kike wengine waliotunga majumbani kwao tu, Khulaita aliamua kujitokeza hadharani. Nyimbo zake zilipendwa na Waswahili popote walipo duniani. Khulaita alitazama jamii yake kwa makini sana na hakuogopa kusema aliyoyaona. Hasa udhalimu na unyonge ulimwudhi kiasi kwamba hakuweza kunyamaza kimya. Alifahamu nguvu na udhaifu wa hadhira yake. Hali hiyo ilimwezesha kuwagusa wasikilizaji.
Kwa sababu alikuwa mtunzi wa kike mwenye sifa ya huruma na akili, wanawake walifika kwake kushauriwa na kutungiwa nyimbo. Kwa hiyo Khulaita alijua vizuri yaliyowashughulisha wanawake. Kupitia tungo zake aliwapa sauti. Ubingwa na umahiri wake ulimruhusu kusema yoyote kwa namna inayokubalika katika jamii.
Kwa kuchambua nyimbo za majibizano makala haya yanamulika jinsi Khulaita alivyotingisha jamii kuhusu maswala ya jinsia.
Stefanie Kolbusa alisoma Lugha za Kiafrika na Anthropolojia Chuo Kikuu cha Bayreuth na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Baada ya kupata shahada ya uzamivu katika Fasihi ya Lugha za Kiafrika chini ya usimamizi wa Said Ahmed Khamis alifundisha Fasihi ya Kiswahili na Anthropolojia nchini Rwanda. Kabla ya kurudi Ujerumani mwaka uliopita alifanya kazi Chuo Kikuu cha Aga Khan London.
Wale ambao mpaka sasa hawako kwenye kikundi cha barua pepe yetu BALAKI-BE wangeweza kutuandikia kwa anwani augustine.malija(at)zmo.de, na watapewa kiunganishi kwa ajili ya kuingia na kushiriki kwenye mazungumzo pamoja na sisi. – Pia kama kuna maswali yoyote kuhusu baraza hili, tafadhali mwandikieni Bwana Augustine Malija kwa anwani tajwa.
Mabaraza yetu yajayo muhula huu yatafanyika tarehe 11 Januari na 8 Februari 2021.
Soma ripoti ya baraza lililopita juu ya Korona na angalia rekordi yake. Pia unaweza kupata habari zifananazo katika ukurasa wetu wa Korona. Mfano hali ya maisha mji wa kale, Mombasa , safari ya Abdilatif Abdallah Afrika Mashariki na mapokeo ya Korona nchini Uganda.
This event is part of the lecture series:
Presentation and Discussion Sessions in Swahili
Baraza la Kiswahili la Berlin
Details
Virtual Event