Kumkumbuka na Kumwenzi Marehemu Euphrase Kezilahabi (1944-2020)
Marehemu Euphrase Kezilahabi alikuwa mwandishi na msomi asiyekuwa na kifani. Mchango wake katika nyanja za ushairi, riwaya, hadithi fupi, tamthilia utakumbukwa daima. Alikuwa mwanafalsafa na mwanafasihi aliyewavutia na kuchochea fikra na hisia za wasomi wenzake na wasomaji wake kwa ujumla. Katika baraza hili, tungependa kumkumbuka na kumwenzi Marehemu Euphrase Kezilahabi kwa pamoja tukiwapa wanatafiti wa rika la ‛vijana’ pamoja na wanafunzi nafasi ya kutoa michango yao.
Wazungumzaji na wenyekiti watakuwa ni Alena Rettová (Profesa wa Falsafa za Kiafrika katika Lugha za Kiafrika, Chuo Kikuu cha Bayreuth), Neema Benson Sway (Mwanafunzi wa Shahada ya Tatu, Taasisi ya Taaluma ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam), Lena Dasch (Mwanafunzi wa Shahada ya Pili, Idara ya Taaluma za Afrika, Chuo Kikuu cha Humboldt Berlin), Josefine Rindt (Mwanafunzi wa Shahada ya Pili, Taasisi ya Taaluma ya Siasa, Chuo Kikuu Huru cha Berlin), Roberto Gaudioso (Mtafiti wa Fasihi ya Kiswahili, Napoli), Erasto John Duwe (Mwalimu na Mhariri, Taasisi ya Taaluma ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) na mwenyeji mmojawapo Luti Diegner (Mhadhiri Mwandamizi wa Lugha na Fasihi ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Humboldt Berlin).
Tutakutana siku ya Jumatatu, tarehe 11/01/2021, saa nane hadi saa kumi na mbili (14-18 hours za huku Berilini), kupitia platfomu ya Zoom mkondoni:
us02web.zoom.us/j/84562158576
Meeting ID: 845 6215 8576
Passcode: 517095
KARIBUNI SANA!
This event is part of the lecture series:
Presentation and Discussion Sessions in Swahili
Baraza la Kiswahili la Berlin
Details
Virtual Event