1. Leibniz-Zentrum Moderner Orient
  2. Events
  3. Lullabies among the Watiku: Content and Meaning
Events
Lecture, Lecture series

Lullabies among the Watiku: Content and Meaning

Swahili Baraza with Rukiya Swaleh (Pwani University, Kilifi)

Ndugu waheshimiwa, wapendwa wanafunzi na marafiki zetu,

Tungependa kuwatangazia kikao kifuatacho cha Baraza letu la Kiswahili la Berlin (BALAKI - BE) ambacho kitakuwa na mada ifuatayo: Bembelezi za Watikuu: Maudhui na Mtindo

Daktari Rukiya Harith Swaleh ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Pwani. Wasilisho hili lake linachunguza bembelezi kama mojawapo wa utanzu wa fasihi simulizi chini ya nyimbo. Kulingana na Swaleh, bembelezi ni utanzu ambao umesahaulika kwani hakuna tafiti nyingi ambazo zinaangazia juu yake. Katika makala haya, Swaleh anajaribu kuangazia maudhui yanayojitokeza wakati wanawake wa Watikuu wanapowabembeleza watoto. Watikuu ni Waswahili wanaoishi sehemu ya kaskazini mwa visiwa vya Lamu na kusini mwa Somalia. Wanawake hawa hutumia fursa ya kuwabembeleza watoto kwa kutoa waliyonayo kwenye roho zao au kuwasilisha ujumbe fulani. Watikuu hawaangalii bembelezi kuwa ni za maudhui ya aina moja bali maudhui ya kila aina huweza kutumika. Mtindo wa lugha unaotumika vilevile hubadilika, mara huwa kuna wingi wa mafumbo, kejeli na sitiari katika nyimbo hizo. Data imekusanywa kutoka kwa wanawake wa Kitikuu kumi kutoka kisiwa cha Kizingitini. Swaleh pia katika kuishi kwake huko ametagusana na bembelezi mbalimbali.

KARIBUNI NYOTE! 

Please register with MaxwellOmondi.Ondieki(at)zmo.de

This event is part of the lecture series:
Presentation and Discussion Sessions in Swahili 2023
Baraza la Kiswahili la Berlin

Details