The Importance of Appreciating Basic Human Names of African Cultures using Paul Ricoeur's Theory
Katika wasilisho hili Dkt. Bin-Kapela atayajadili kwa undani maana fichika ya majina ya binadamu yenye asili ya mila za Kiafrika. Anazingatia mtazamo wa kihistoria kueleza jinsi, katika enzi ya utumwa, majina haya yalifutwa ili watumwa wapoteze kumbukumbu ya tamaduni zao. Pia yalifutwa kuwabagua na kuwadunisha watu wenye asili ya Kiafrika yaani kuwanyima hadhi ya kuwa binadamu kama wenzao wengine. Baadaye hayo majina ya Kiafrika yalibadilishwa kuwa majina ya Kizungu. Baada ya uhuru, viongozi wa nchi za Afrika walianzisha itikadi ya kuthamini tamaduni zao, ikiwemo kurejesha majina yao ya jadi. Dkt. Bin-Kapela atafafanua kuwa majina hayo yana muundo rudufu yaani yana maana bayana na maana fichika. Kwa kutumia nadharia ya Paul Ricoeur atafichua thamani iliyopo katika maana fichika ya majina hayo.
Victor Badibanga Bin-Kapela ana shahada za Chuo Kikuu cha Lubumbashi na shahada ya udaktari wa falsafa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Amefundisha masomo ya falsafa katika vyuo vikuu mbalimbali toka mwaka 1990. Pia ameandika vitabu na makala kadhaa kwenye uwanja wa tafsiri ya utamaduni.
Kikao kitafanyika siku ya Jumatatu, tarehe 03 Juni 2024, saa kumi kamili za Ulaya ya Kati (saa kumi na moja za Afrika Mashariki) kupitia njia ya Zoom: Kikao kitafanyika siku ya Jumatatu, tarehe 03 Juni 2024, saa kumi kamili za Ulaya ya Kati (saa kumi na moja za Afrika Mashariki) kupitia njia ya Zoom: https://us02web.zoom.us/j/89156449097?pwd=NAIDpi6DSWR5QpS6SNZFa0HA21Llvp.1
KARIBUNI NYOTE!
Tafadhalini wajulisheni wapenzi wote wa Kiswahili na marafiki wengine!
Wasalaam,
Kai Kresse, Lutz Diegner na Maxwell Omondi Ondieki
Kama kuna maswali yoyote kuhusu baraza hili tafadhalini mwandikieni mwenzetu: MaxwellOmondi.Ondieki(at)zmo.de
This event is part of the lecture series:
Presentation and Discussion Sessions in Swahili 2024
Baraza la Kiswahili la Berlin
Details
online