1. Leibniz-Zentrum Moderner Orient
  2. Events
  3. The Importance of Arrangement of Terms in Swahili Sentences
Events
Lecture

The Importance of Arrangement of Terms in Swahili Sentences

Swahili Baraza with Mussa Amanzi (Muslim University of Morogoro)

Ndugu waheshimiwa, wapendwa wanafunzi na marafiki zetu,

Baada ya wingi wa salamu ni furaha yetu kubwa kutangaza kikao kifuatacho cha Baraza letu la Kiswahili la Berlin (BALAKI‐BE) la tarehe 11 Julai 2022: Umuhimu wa Uzingativu wa Mpangilio wa Viseme katika Tungo za Kiswahili

Mussa Amanzi
Wasilisho hili la Mussa Amanzi linakusudia kuonesha umuhimu wa kupangilia viseme katika sentensi ili kupata maana sahihi kama inavyohitajika kimawasiliano. Amanzi anasema kwamba waandishi wengi hukosea kufikisha ujumbe kitaalamu kwa sababu ya kutokujua ni wapi hasa kiseme hutakiwa kuwekwa ili kutimiza lengo hilo la kimawasiliano. Kulingana naye Amanzi, kuna nafasi tatu zinazokaliwa na viseme katika sentensi za lugha ya Kiswahili ambazo ni nafasi ya mwanzo, nafasi ya kati na nafasi ya mwishoni. Kila nafasi ina jukumu lake la kipekee katika kuunda maana ya sentensi hiyo. Kushindwa kujua majukumu hayo kunapelekea kupanga hovyo viseme hivyo na hatimaye kupatikana maana isiyoeleweka yenye ukakasi na uvulivuli n.k. Viseme vinavyounda nafasi hizo tatu huhamahama na kuacha nafasi yake ya asili kutokana na sababu za kimaana na kimuundo. Kujua sababu hizo ni muhimu mno katika kuwasilisha maana ipasavyo, asemaye Amanzi. Kwa hiyo wasilisho lake linajitahidi kuwasaidia wasomi katika kuandika kwa kupangilia ipasavyo viseme hivyo katika sentensi.

Daktari Mussa Omari Amanzi ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro nchini Tanzania. Makazi yake ni Idara ya Kiswahili- Isimu. Tasinifu zake zimejiegemeza katika uwanja wa Sintaksia ya Kiswahili. Ameandika vitabu vinne vya Isimu vinavyohusu Semantiki, Fonolojia, Mofolojia na Utangulizi wa Isimu.

Kikao kitafanyika siku ya Jumatatu, tarehe 11 Julai 2022, saa kumi kamili za Ulaya ya Kati (saa kumi na moja za Afrika Mashariki) kupitia njia ya Zoom: https://tinyurl.com/26f9cu96

KARIBUNI NYOTE! 

Tafadhalini wajulisheni wapenzi wote wa Kiswahili na marafiki wengine!

Wasalaam,
Kai Kresse, Lutz Diegner na Maxwell Omondi Ondieki

Kama kuna maswali yoyote kuhusu baraza hili tafadhalini mwandikieni mwenzetu: MaxwellOmondi.Ondieki(at)zmo.de

This event is part of the lecture series:
Presentation and Discussion Sessions in Swahili 2022
Baraza la Kiswahili la Berlin

Details