1. Leibniz-Zentrum Moderner Orient
  2. Events
  3. Vijitabu Vilivyopita bahari kuu. Uchapishaji wa Kiswahili wa Kiislamu na mtandao wake katika karne ya ishirini.
Events
Lecture

Vijitabu Vilivyopita bahari kuu. Uchapishaji wa Kiswahili wa Kiislamu na mtandao wake katika karne ya ishirini.

Tukiongozwa na Annachiara Raia, ataangazia historia ya uchapishaji wa vijitabu vya kiisilamu katika Kiswahili na historia yake kama ifuatavyo.

Inajulikana kuwa historia ya utamaduni wa uchapishaji imeathiri maendeleo ya jamii na fasihi duniani. Suala ambalo nitashughulika nalo katika wasilisho hili ni kuhusu historia na namna vijitabu vya Kiswahili vya Kiislamu vilivyosafiri, na vilivyochapishwa Afrika Mashariki. Kuanzia karne ya ishirini, uchapishaji wa Kiislamu ulianza kuenea na kujenga mawasiliano kati ya wasomaji na waandishi kutoka Afrika Mashariki na Bahari Kuu. Nitaonyesha uhusiano baina ya vijitabu hivi na nyumba zao za uchapishaji. Kwa njia hii nitaeleza vipengele vya mtandao wa vitabu, wauzaji kutoka maduka ya mijini Mombasa na Nairobi na nyumba za uchapishaji kutoka Bahari Kuu. Kama magazeti mengine ya Kiislamu yenye habari, lengo la vijitabu vya Kiswahili vya Kiislamu ni kuelimisha umma kuhusu nyanja mbalimbali, kama historia ya Uislamu, tafsiri za kidini na fasihi ya Kiswahili.

Annachiara Raia ni mwalimu wa Fasihi ya Kiafrika Chuo Kikuu cha Leiden. Fani yake ni fasihi ya Kiswahili ya Kiislamu na anashugulika na fasihi simulizi na fasihi andishi. Alipata shahada yake ya tatu kwa kuandika tasnifu kuhusu historia ya Utendi wa Yusuf akisomea Chuo Kikuu cha Bayreuth. Siku hizi anandika kitabu kuhusu mashairi ya Mahmoud Mau.

Join Zoom Meeting:
us02web.zoom.us/j/83656870598
Meeting ID: 836 5687 0598
Passcode: 390554

This event is part of the lecture series:
Presentation and Discussion Sessions in Swahili
Baraza la Kiswahili la Berlin

Details