Visa na Mikasa ya akina Osale na Paulo huko Usambaani Tanzania Miaka ya 1950
Lecture by Stephanie Lämmert
Katika wasilisho langu nitazungumzia visa na mikasa ya wanaume wawili, kwa majina Osale Otango na Paulo Hamisi, walioishi nchini Tanzania wakati wa ukoloni. Bwana Osale na Bwana Paulo walileta changamoto kubwa kwa masetla wa Usambaani kwa sababu waliingia katika nyumba zao usiku na kuwatishia, muda mwingine na kuiba. Walijulikana kama majambazi kwa wakoloni na masetla wa Usambaani. Lakini wenyeji wa Usambaani waliwaona kama watu wenye lengo la kupigania uhuru na kumwondoa mkoloni. Katika utafiti wangu niliwahoji wakazi wa Usambaani kujifunza zaidi kuhusu maisha na kifo cha Bwana Osale na Bwana Paulo, na pia kuelewa siri yao ya kufanikiwa kutoonekana kwa maadui wao. Nimepata kuelewa kuwa kisa cha Bwana Osale na Bwana Paulo kwa kweli ni kisa cha kupinga mfumo msonge wa ubaguzi wa rangi wakati wa ukoloni. Pia kisa hicho kinaonyesha umuhimu wa utafiti wa historia simulizi.
Dk. Stephanie Lämmert ni mtafiti wa historia ya Afrika katika Taasisi ya Maendeleo ya Binadamu Max Planck hapa Berlin. Alifanya utafiti kuhusu historia ya Usambaani, Tanzania, wakati wa ukoloni. Siku hizi anajishughulisha na historia ya ndoa ya wenyeji wa Ukanda wa Shaba huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia.
Kikao kitafanyika saa kumi kamili za huku (saa kumi na moja kamili za Afrika Mashariki) hadi saa kumi na mbili kasoro (saa moja kasoro za Afrika Mashariki) kwa njia ya Zoom.
Join Zoom Meeting:
https://us02web.zoom.us/j/87506967125?pwd=em4wdEFoNVZCMFp2ZTlkUzEraDBFZz09
Kama kuna maswali yoyote kuhusu baraza hili tafadhalini mwandikieni mwenzetu: <augustine.malija@zmo.de>
This event is part of the lecture series:
Presentation and Discussion Sessions in Swahili
Baraza la Kiswahili la Berlin
Details
ZMO / Online