1. Leibniz-Zentrum Moderner Orient
  2. Events
  3. WASWAHILI (VIJANA) WA OMAN NA DHANA YA “ZANZIBAR DIASPORA”
Events
Lecture

WASWAHILI (VIJANA) WA OMAN NA DHANA YA “ZANZIBAR DIASPORA”

Tukiongozwa na Franziska Fay amabye atajibu maswali juu ya utafiti wake kama ifuatavyo.

Maana yake nini kuwa kijana (chini ya umri wa miaka 35) anayezungumza Kiswahili nchini Oman? Vijana wale wanajitambuaje kivipi katika muktadha wa inayoitwa ‘Zanzibari Diaspora’? Kwa njia gani kuwa Omani na kuwa Mswahili yanaenda sambamba? Ninapoanza na mradi mpya wa utafiti wangu wa kianthropolojia naomba nitumie nafasi ya BALAKI-BE kutafakari kuhusu maswali hayo na kukusanya maoni tofauti ya wale wanaoathirika na fikra hizo. Mazingatio yangu yanajengwa kwenye wiki chache ya utafiti wa awali nchini Oman na Zanzibar mwaka 2018/2019.
Franziska Fay ni postdoctoral researcher wa anthropolojia katika kituo cha utafiti kiitwacho “Normative Orders” kilichopo katika chuo kikuu cha Goethe mjini Frankfurt. Alikamilisha PhD yake chuo kikuu cha SOAS, London, na kwa miezi ya Oktoba mpaka Disemba 2020 yeye ni Visiting Researcher on the Omani Fellowship katika ZMO Berlin. Unaweza kupata taarifa zake zaidi hapa.

https://www.franziskafay.com/

KARIBUNI SANA!

Tafadhalini wajulisheni wapenzi wote wa Kiswahili na marafiki wengine!

PS. Wale ambao mpaka sasa hawako kwenye kikundi cha barua pepe yetu BALAKI-BE wangeweza kutuandikia kwa anwani augustine.malija@zmo.de, na watapewa kiunganishi kwa ajili ya kuingia na kushiriki kwenye mazungumzo pamoja na sisi. – Pia kama kuna maswali yoyote kuhusu baraza hili, tafadhali mwandikieni Bwana Augustine Malija kwa anwani tajwa.
 

This event is part of the lecture series:
Presentation and Discussion Sessions in Swahili
Baraza la Kiswahili la Berlin

Details