1. Leibniz-Zentrum Moderner Orient
  2. Veranstaltungen
  3. Bembelezi za Watikuu: Maudhui na Mtindo
Veranstaltungen
Vortrag, Vortragsreihe

Bembelezi za Watikuu: Maudhui na Mtindo

Swahili Baraza mit Rukiya Swaleh (Chuo Kikuu cha Pwani, Kilifi)

Um den Teilnahmelink zu erhalten, senden Sie bitte eine Email an MaxwellOmondi.Ondieki(at)zmo.de

Ndugu waheshimiwa, wapendwa wanafunzi na marafiki zetu,

Tungependa kuwatangazia kikao kifuatacho cha Baraza letu la Kiswahili la Berlin (BALAKI - BE) ambacho kitakuwa na mada ifuatayo: Bembelezi za Watikuu: Maudhui na Mtindo (Lullabies among the Watikuu: Content and Meaning)

Daktari Rukiya Harith Swaleh ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Pwani. Wasilisho hili lake linachunguza bembelezi kama mojawapo wa utanzu wa fasihi simulizi chini ya nyimbo. Kulingana na Swaleh, bembelezi ni utanzu ambao umesahaulika kwani hakuna tafiti nyingi ambazo zinaangazia juu yake. Katika makala haya, Swaleh anajaribu kuangazia maudhui yanayojitokeza wakati wanawake wa Watikuu wanapowabembeleza watoto. Watikuu ni Waswahili wanaoishi sehemu ya kaskazini mwa visiwa vya Lamu na kusini mwa Somalia. Wanawake hawa hutumia fursa ya kuwabembeleza watoto kwa kutoa waliyonayo kwenye roho zao au kuwasilisha ujumbe fulani. Watikuu hawaangalii bembelezi kuwa ni za maudhui ya aina moja bali maudhui ya kila aina huweza kutumika. Mtindo wa lugha unaotumika vilevile hubadilika, mara huwa kuna wingi wa mafumbo, kejeli na sitiari katika nyimbo hizo. Data imekusanywa kutoka kwa wanawake wa Kitikuu kumi kutoka kisiwa cha Kizingitini. Swaleh pia katika kuishi kwake huko ametagusana na bembelezi mbalimbali.

KARIBUNI NYOTE! 

–––––

Doctor Rukiya Harith Swaleh is a lecturer at Pwani University. This presentation by Rukiya Harith Swaleh examines lullabies as an aspect of oral traditions and culture. According to Swaleh, the performance of lullabies as credible purveyors of traditional culture is fast dying out due to neglect. As a countermeasure, Swaleh analyses the language which informs the meaning of lullabies among the Watikuu, the northern Swahili who populate the mainland north-eastward of Lamu close to Somalia. The content of lullabies reflect the ability of Watikuu women to use verbal texts as a medium to blend the realities of their everyday lives with their overall cultural expectations. The purpose of lullabies derive much of their meaning from the aesthetics, imagery and satire embedded in the songs. The data used in this research was collected from a group of ten women resident in the port of Kizingitini. This was analysed in tandem with Swaleh’s own personal experience with lullabies.

KARIBUNI NYOTE! 

Diese Veranstaltung gehört zur Vortragsreihe
Swahilisprachige Veranstaltungsreihe 2023
Baraza la Kiswahili la Berlin

Veranstaltungsdetails