1. Leibniz-Zentrum Moderner Orient
  2. Veranstaltungen
  3. HipHop as a Medium for Transmitting Cultural Values in Tanzania
Veranstaltungen
Kulturveranstaltung, Vortrag

HipHop as a Medium for Transmitting Cultural Values in Tanzania

Swahili Baraza mit Mutalemwa Jason Mushumbusi (Maalim Nash)

Ndugu waheshimiwa, wapendwa wanafunzi na marafiki zetu,

Baada ya muhula wa huku kuanza ni furaha yetu kubwa kutangaza kikao kifuatacho cha Baraza letu la Kiswahili la Berlin (BALAKI-BE) ambacho kitakuwa na mada ifuatayo: Vidokezo vya Harakati za Ukuzaji wa Lugha ya Kiswahili Kisilisila na Kiwima

Baada ya kongamano letu zuri la wiki jana ni furaha yetu kubwa kutangaza kikao kifuatacho cha Baraza letu la Kiswahili la Berlin (BALAKI-BE) la tarehe 05 Juni 2023: Mchango wa HipHop katika Kujenga Jamii yenye Maadili Nchini Tanzania (Kikao na Konsati Fupi)

Mutalemwa Jason Mushumbusi (Maalim Nash)

Katika wasilisho hili, Maalim Nash anatumia nyimbo zake kama rejea kuyadili majukumu mbalimbali ambayo muziki wa HipHop unatekeleza katika jamii. Lengo kuu la muziki wake wa HipHop ni la kuiburudisha na hata kuielimisha jamii. Kutokana na kutumia HipHop katika kuielemisha jamii, Nash anaeleza hali ya maadili nchini Tanzania, na jinsi muziki wa HipHop unavyoweza kutumika kueneza ujumbe wa amani, usawa na umoja katika jamii. Aidha, atatoa mapendekezo kwa nchi za Afrika kuupa muziki wa HipHop nafasi zaidi kwa kuutumia kama chombo cha kufundishia kwenye somo la maadili. Hatimaye, Nash anatoa wito kwa mataifa ya magharibi kuthamini na kuheshimu tamaduni za Kiafrika akiongezea kwamba maadili ni jambo la kitamaduni na kila jamii ina tamaduni zake.

Maalim Nash ni msanii wa HipHop aliyeingia ulingoni akiwa bado kijana. Ametoa albamu nyingi zikiwemo Mzimu wa Shaaban Robert, Mchochezi na Mhadhiri. Ameshiriki na kuanzisha harakati mbalimbali kwa ajili ya kujadili uhusiano wa lugha na maarifa kama Kiswahili na Sanaa (KINASA), TAMADUNI MUZIK, SUA (Serving Underground Artists), na SANAA KWA MANUFAA. Amewahi kualikwa vyuo vikuu vya North Carolina na Bayreuth na vilevile alipiga nyimbo zake Afrika Kusini na Berlin.

Kikao kitafanyika siku ya Jumatatu, tarehe 05 Juni 2023, saa kumi kamili za Ulaya ya Kati (saa kumi na moja za Afrika Mashariki) Zentrum Moderner Orient, Kirchweg 33, 14129 Berlin. Pia kitapatikana kupitia njia ya Zoom:

https://us02web.zoom.us/j/87403517259?pwd=SDZNSmNoS3AybitaL3N4VWNPWEEzUT09

Baada ya kikao kutakuwa na konsati fupi ya Maalim Nash akituonjesha sanaa yake. Tunatarajia kuwa na sherehe ndogo baadaye, kwa hivyo mjipange vilivyo tukawe wote muda mrefu zaidi jioni hiyo.

KARIBUNI NYOTE!

Tafadhalini wajulisheni wapenzi wote wa Kiswahili na marafiki wengine!

Wasalaam,
Kai Kresse, Lutz Diegner na Maxwell Omondi Ondieki

Kama kuna maswali yoyote kuhusu baraza hili tafadhalini mwandikieni mwenzetu: MaxwellOmondi.Ondieki(at)zmo.de

Diese Veranstaltung gehört zur Vortragsreihe
Swahilisprachige Veranstaltungsreihe 2023
Baraza la Kiswahili la Berlin

Veranstaltungsdetails