1. Leibniz-Zentrum Moderner Orient
  2. Veranstaltungen
  3. Narratives of Migration from East Africa to the Arabian Gulf during the decades of the 1960s and 1970s
Veranstaltungen
Vortrag

Narratives of Migration from East Africa to the Arabian Gulf during the decades of the 1960s and 1970s

Swahili Baraza with Nathaniel Mathews (Binghamton University)

Ndugu waheshimiwa, wapendwa wanafunzi na marafiki zetu,

Baada ya mwezi wa mapumziko ni furaha yetu kubwa kutangaza kikao kifuatacho cha Baraza letu la Kiswahili la Berlin (BALAKI - BE) ambacho kitakuwa na mada ifuatayo: Masimulizi ya Uhamiaji kutoka Afrika Mashariki kwenda Ghuba ya Kiarabu wakati wa miongo 1960 - 1970 - Nathaniel Mathews (Chuo Kikuu cha Binghamton)

Katika wasilisho hili Profesa Mathews atayajadili masuala yanayotoka kwenye utafiti aliyefanya 2012 - 2013 mjini Muscat nchini Oman na WaOmani waliozaliwa Afrika Mashariki, pamoja na utafiti aliyefanya 2014 kwenye nyaraka za taifa Zanzibar na nyaraka nyingine mbalimbali. Maisha ya wahamiaji katika kipindi hiki yanaonyesha michakato minne ya uhamiaji. Kwanza, “Wamanga” waliotoroka Zanzibar kama wakimbizi 1964 - 1965 baada ya mapinduzi ya Zanzibar. Wengi wao walisaidiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Huduma za Wahamiaji (UNHCR) na Msalaba Mwekundu kuingia Oman, na wengine walihamia pahali pengine: Dubai, Abu Dhabi, Doha, na Dammam, Saudi Arabia. Pili, miongo ya Wazanzibari waliotoroka Zanzibar kwa siri mwisho wa 1960 hadi mwanzo wa 1970. Wao walijaribu kupata uraia au kibali cha makao ya kudumu kwenye nchi za Ghuba. Tatu, raia ya Afrika Mashariki waliohamia Ghuba kutafuta kazi: wahamiaji wa kazi ya muda. Na mchakato wa mwisho ni Waarabu WaOmani wanaokaa Tanzania na nchi zingine za Afrika Mashariki. Wao waliitikia mwaliko wa Sultan Quaboos waje Oman kusaidia kujenga taifa baada ya mwaka 1970.

Nathaniel Mathews ni Profesa Mshirikishi katika Idara ya Masomo ya Kiafrika, Chuo Kikuu cha Binghamton, Amerika. Alipata shahada ya udaktari katika Historia kutoka Chuo Kikuu cha Northwestern mnamo 2016.

Kikao kitafanyika siku ya Jumatatu, tarehe 09 Mei 2022, saa kumi kamili za Ulaya ya Kati (16 CET) kupitia njia ya Zoom: https://tinyurl.com/4t73a273

Mkiwa na maswali karibuni mtuandikie baruapepe: <MaxwellOmondi.Ondieki@zmo.de >

 

KARIBUNI NYOTE!

Tafadhalini wajulisheni wapenzi wote wa Kiswahili na marafiki wengine!

Wasalaam,

Kai Kresse, Lutz Diegner na Maxwell Omondi Ondieki

Diese Veranstaltung gehört zur Vortragsreihe
Swahilisprachige Veranstaltungsreihe 2022
Baraza la Kiswahili la Berlin

Veranstaltungsdetails