1. Leibniz-Zentrum Moderner Orient
  2. Veranstaltungen
  3. Performance Context of Jokes in Hehe Society
Veranstaltungen
Vortrag

Performance Context of Jokes in Hehe Society

Swahili Baraza with Asifiwe Mwagike (Dar es Salaam University)

Ndugu waheshimiwa, wapendwa wanafunzi na marafiki zetu,

Tungependa kuwatangazia kikao kifuatacho cha Baraza letu la Kiswahili la Berlin (BALAKI - BE) ambacho kitakuwa na mada ifuatayo: Utendaji wa Utani katika Jamii ya Wahehe

Asifiwe Mwagike (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam)

Katika wasilisho hili Mwalimu Asifiwe Mwagike atatuelemisha kuhusu utani ambayo ni kipera cha mazungumzo/nyambi katika fasihi simulizi chenye dhima mbalimbali kwa jamii husika. Lengo la utafiti huu ni kuchunguza mikitadha, mbinu na dhima za utendaji wa utani katika jamii ya Wahehe. Maswali anayekumbana nayo ni: Je, ni miktadha ipi inayohusishwa na utendaji wa utani katika jamii ya Wahehe? Ni mbinu zipi zinazotumika wakati wa utendaji wa utani? Nini dhima ya utendaji huo wa utani katika jamii hii? Data za utafiti huu zimekusanywa na Mwalimu Mwagike kwa kutumia mbinu ya mahojiano na ushuhudiaji wa misiba vilevile harusi na kuchambuliwa kwa kutumia Nadharia ya Utendaji na Sosholojia ya Fasihi. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa utendaji wa utani hujibainisha zaidi msibani na harusini. Aidha, utendaji wa utani huo hutumia mbinu ya kumuanika nje mfiwa, majibizano, nyimbo, masimulizi na maleba pamoja na vifaa vyake. Utendaji huo wa utani huwa na dhima kama vile kudumisha umoja na ushirikiano, kupunguza majonzi kwa wafiwa, kuilinda amali hii muhimu ya utani miongoni mwa wanajamii, kuonya, kutoa mafunzo ya ndoa kwa vijana, kuhimiza ufanyaji kazi pamoja na kuburudisha.

Asifiwe Mwagike anasomea shahada ya uzamivu akifanya kazi Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CKD). Hatua aliyoifikia hadi sasa ni ya uchanganuzi wa data. Muhula huu amepewa skolashipu ya Idara ya Taaluma za Afrika ya Chuo Kikuu cha Humboldt akiendeleza utafiti wake hapa Berlin.

Kikao kitafanyika muundo mseto siku ya Jumatatu, tarehe 27 Juni 2022, saa kumi na robo za Ulaya ya Kati (saa kumi na moja na robo za Afrika Mashariki) katika Idara ya Taasisi ya Taaluma za Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Humboldt (Chumba namba 410), Invalidenstrasse 118, 10115 Berlin.
Zoom: https://tinyurl.com/bdtaec24

KARIBUNI NYOTE!

Tafadhalini wajulisheni wapenzi wote wa Kiswahili na marafiki wengine!

Wasalaam,
Kai Kresse, Lutz Diegner na Maxwell Omondi Ondieki

Kama kuna maswali yoyote kuhusu baraza hili tafadhalini mwandikieni mwenzetu: MaxwellOmondi.Ondieki(at)zmo.de

 

Diese Veranstaltung gehört zur Vortragsreihe
Swahilisprachige Veranstaltungsreihe 2022
Baraza la Kiswahili la Berlin

Veranstaltungsdetails