1. Leibniz-Zentrum Moderner Orient
  2. Veranstaltungen
  3. Ndoa, Utumwa, na Sauti za Wanawake katika Tanganyika ya Kikoloni
Veranstaltungen
Vortragsreihe

Ndoa, Utumwa, na Sauti za Wanawake katika Tanganyika ya Kikoloni

Ndoa, Utumwa, na Sauti za Wanawake katika Tanganyika ya Kikoloni 
Dkt. Saada Omar Wahab

Wakati baadhi ya tafiti za kihistoria zimewaonyesha wanawake wa Kiafrika kama wasio na sauti 
katika mijadala kuhusu utumwa na ndoa, wasilisho hili linapinga dhana hiyo kwa kutoa ushahidi 
mbadala. Katika kipindi cha baada ya kukomeshwa kwa biashara ya utumwa na utumwa kisheria 
katika Tanganyika ya kikoloni, mijadala kuhusu ndoa iliendelea kubeba taswira na mantiki 
zinazokaribiana na zile za utumwa. Ndani ya muktadha huo, wasilisho hili linachunguza jinsi 
wanawake walivyotumia uzoefu wa ndoa kueleza masuala ya mamlaka, utegemezi, na uhuru. 
Uchambuzi unategemea makala zilizochapishwa kati ya miaka ya 1925 na 1926 katika gazeti la 
Kiswahili Mambo Leo, hususan makala mbili za Zeina Mwinyipembe, zikionyesha jinsi wanawake 
walivyojadili ndoa kwa kutumia lugha na mifano inayorejelea utumwa. Aidha, uchambuzi 
unazingatia mila, matendo, na mahusiano ya kijinsia yaliyoakisi dhana za umiliki ndani ya ndoa. 
Wasilisho linaonyesha ndoa kama muendelezo wa mifumo ya ukosefu wa uhuru iliyohusishwa na 
historia ya utumwa. 

Dkt. Saada Omar Wahab ni Mhadhiri na Mtafiti wa historia katika Chuo Kikuu cha Taifa cha 
Zanzibar (SUZA). Ana Shahada ya Uzamivu katika Sayansi Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Göttingen, 
Ujerumani. Utafiti wake unajikita katika historia ya wanawake watumwa, diaspora ya Zanzibar, na 
umiliki wa ardhi. Kwa sasa, anahusika na utafiti unaochunguza sauti za wanawake katika muktadha 
wa utumwa na ndoa nchini Tanzania. 

Kikao kitafanyika siku ya Jumatatu, tarehe 06 Julai 2026, saa kumi na robo za Ulaya ya Kati 
(saa kumi na moja na robo za Afrika Mashariki) kupitia njia ya Zoom:

us02web.zoom.us/j/83313825142
 

Veranstaltungsdetails