Swahilisprachige Veranstaltungsreihe Sommer 2026
Vortragsreihe
Wajuzi waheshimiwa, wapendwa wanafunzi na marafiki zetu,
Baada ya muda mrefu wa mapumziko, ni furaha yetu kubwa kuwatangazia ratiba ya muhula huu mpya wa Baraza la Kiswahili la Berlin (BALAKI-BE). Tunatarajia kuwa na vikao vitatu kipindi hiki. Tafadhali zingatieni tarehe zifuatazo:
- 4 Mei 2026, Jumatatu saa kumi na robo (saa kumi na moja na robo za Afrika Mashariki) Dkt. IZABELA ROMAŃCZUK wa Chuo Kikuu cha Warsaw, Uzinduzi wa Kitabu: ‘Riwaya za Kiswahili za Waandishi Wanawake wa Tanzania: Wakala, Mapokeo na Mabadiliko’ (2025)
- 08 Juni 2026, Jumatatu, saa kumi na robo (saa kumi na moja na robo za Afrika Mashariki)
Prof. AMANDINA LIHAMBA wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (Mada inasubiriwa) - 06 Julai 2026, Jumatatu, saa kumi na robo (saa kumi na moja na robo za Afrika Mashariki).
Taarifa za mwasilishaji na mada bado hazijathibitishwa
Vikao vyote vitafanyika kupitia Zoom. Matangazo na viunganishi vitasambazwa kabla ya kila kikao.
KARIBUNI NYOTE!