Mabadiliko ya Maisha Kipindi cha Ugonjwa wa Korona: Life Changes in Times of Corona
Tukiongozwa na wazungumzaji wetu Profesa Nandera Mhando (Dar es Salaam), mwandishi Abdilatif Abdalla (Hamburg), Profesa Hassan Mwakimako (Mombasa) na Prof Nicholas Githuku (New York) tutazungumza jinsi mfumo wa maisha ulivyobadilika kipindi hiki cha Korona. Wazungumzaji watatueleza juu ya changamoto walizokutana nazo na jinsi gani hasa zilivyoyaathiri maisha yao binafsi, familia na jamii zinazowazunguka. Haswa haswa, watazungumzia njia za kibunifu na za kitahadhari ambazo wao na jamii zao wamezibuni ili kujiepusha na ugonjwa huu. Karibuni mzuru tovuti ya ZMO mtakapokuta mkusanyiko wa michango mbalimbali kuhusu uzoefu wa Korona duniani kote, na miongoni mwake yamo mazungumzo na Abdilatif Abdalla kuhusu safari yake ndefu Afrika Mashariki hivi karibuni: https://www.zmo.de/wissenstransfer/corona-experiences Karibuni pia mpokee taarifa za wasifu wa wazungumzaji wetu katika viunganishi vifuatavyo:
Nandera Mhando, Head of Department, Philosophy and Religious Studies, University of Dar es Salaam
Abdilatif Abdalla, mwandishi wa “Sauti ya Dhiki” (Oxford University Press 1973)
Hassan Mwakimako, Associate Professor of Religious Studies, Pwani University Kilifi, Kenya
Nick Githuku, Assistant Professor of History, Philosophy and Anthropology, York College, CUNY, New York
Tutakutana siku ya Jumatatu, tarehe 06/07/2020, saa kumi kamili, mtandaoni kupitia ‘Zoom’ – tutawatumia kiunganishi wiki moja kabla. KARIBUNI SANA! Tafadhalini wajulisheni wapenzi wote wa Kiswahili na marafiki wengine! Wasalaam, Augustine Malija, Kai Kresse na Luti Diegner
PS. Wale ambao mpaka sasa hawako kwenye kikundi cha barua pepe yetu BALAKI-BE wangeweza kutuandikia kwa anwani augustine.malija@zmo.de, na watapewa kiunganishi kwa ajili ya kuingia na kushiriki kwenye mazungumzo pamoja na sisi. – Pia kama kuna maswali yoyote kuhusu baraza hili, tafadhali mwandikieni Bwana Augustine Malija kwa anwani tajwa.
This event is part of the lecture series:
Presentation and Discussion Sessions in Swahili
Baraza la Kiswahili la Berlin
Details
Virtual presentation