Miaka 50 ya Somo la Fasihi ya Kiswahili Baada ya Uhuru
Farouk Topan
Katika kikao hiki tutazungumzia vipengele vinne vya fasihi ya Kiswahili namna vilivyotiririka tangu miaka ya 1960 hadi miongo miwili ya karne hii. Cha kwanza, vile fasihi ya Kiswahili ilivyofundishwa na kuwekwa imara nje ya Afrika ya Mashariki (hata kabla ya kipindi cha miaka hii); pili, ilivyofundishwa na kujengwa (na pengine kujengeka) Afrika ya Mashariki; tatu, mjaribio wa kuunda nadharia ya/za fasihi ya Kiswahili; na nne, ukuzaji wa fasihi ya Kiswahili na mwingiliano wake na fasihi zingine katika maeneo mbali mbali ya kitaalamu na nadharia.
Farouk Topan ni mwandishi na msomi mashuhuri wa lugha, utamaduni na fasihi ya Kiswahili. Alianzisha kufundisha somo la fasihi ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1968. Amesomesha pia vyuo vikuu vya Nairobi, Riyad, London (SOAS) na sasa yupo Chuo Kikuu cha Aga Khan, huko huko London. Kazi zake za kubuni ni tamthilia na hadithi fupi. Tamthilia zake tatu ni Mfalme Juha (1971), Aliyeonja Pepo (1973), na Siri (2000). Ni furaha yetu kubwa sana kuwa Mwalimu Farouk ameukubali mwaliko wetu atuelimishe katika kikao hiki cha BALAKI-BE.
Kikao kitafanyika saa kumi kamili za huku (saa tisa kamili za Afrika Mashariki) hadi saa kumi na mbili kasoro (saa kumi na moja kasoro za Afrika Mashariki) kwa njia ya Zoom:
https://us02web.zoom.us/j/88159035726?pwd=K0phVDIzRTNnT25Wb0tpL2Fod1d1UT09
KARIBUNI SANA!
Tafadhalini wajulisheni wapenzi wote wa Kiswahili na wenzenu wengine!
Kama kuna maswali yoyote kuhusu baraza hili tafadhalini mwandikieni mwenzetu: <augustine.malija@zmo.de>
This event is part of the lecture series:
Presentation and Discussion Sessions in Swahili
Baraza la Kiswahili la Berlin
Details
ZMO / Online