1. Leibniz-Zentrum Moderner Orient
  2. Veranstaltungen
  3. Uhusiano na Mustakabali wa Fasihi za Kiafrika na Fasihi Nyinginezo Duniani
Veranstaltungen

Uhusiano na Mustakabali wa Fasihi za Kiafrika na Fasihi Nyinginezo Duniani

Profesa Mohamed Bakari ni Makamu Mkuu (Vice-Chancellor) wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Kenya, Nairobi. Alikuwa Profesa wa Kiingereza na Fasihi Baada ya Ukoloni kwenye Chuo Kikuu cha Fatih, Istanbul, Uturuki, kwa miaka mingi. Kabla ya hapo alifundisha katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwa muda mrefu. Kwa ajili ya kuendeleza utafiti wake amewahi kualikwa pembe nyingi duniani kama vile Los Angeles, Oxford, Bayreuth, na Berlin. Kati ya vitabu vyake ni "The Morphophonology of Kenyan Swahili Dialects" (1985), "Islam in Kenya" (1995) na "The Sage of Moroni" (2018), ambacho kinahusu maisha na mawazo ya Said omar Abdalla. Ni furaha yetu kubwa sana kuwa Profesa Bakari amekubali mwaliko wetu atuelimishe katika kikao hiki cha BALAKI-BE.

Kikao kitafanyika saa kumi kamili za huku (saa kumi na mbili za Afrika Mashariki) hadi saa kumi na mbili kasoro (saa mbili kasoro za Afrika Mashariki) kwa njia ya Zoom.

h_ps://us02web.zoom.us/j/89448868985?pwd=RzhkMzRYQ2trSEduZk13RWVsNEd2dz09

 

KARIBUNI SANA

Tafadhalini wajulisheni wapenzi wote wa Kiswahili na wenzenu wengine.

Wasalaam,

Kai Kresse, Luti Diegner na Maxwell Omondi

Kama kuna maswali yoyote kuhusu baraza hili tafadhalini mwandikieni mwenzetu:

MaxwellOmondi.Ondieki@zmo.de

Einladung

Diese Veranstaltung gehört zur Vortragsreihe
Swahilisprachige Veranstaltungsreihe
Baraza la Kiswahili la Berlin

Veranstaltungsdetails