06th July 2020
Hassan Mwakimako (Profesa wa Masomo ya Dini, Chuo Kikuu cha Pwani, Kilifi, Kenya), Nandera Mhando (Mkuu wa Idara, Falsafa na Masomo ya Dini, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam), Nicholas Githuku (Profesa Msaidizi, Historia, Falsafa na Anthropolojia, Chuo Kikuu cha York, CUNY, New York), Neema Kasabo (Mhadhiri wa Kiswahili, Chuo Kikuu Huru, Berlin)
Baraza liliandaliwa na kutambulishwa na Kai Kresse (Mkurugenzi Msaidizi ZMO na Profesa wa Anthropolojia ya Jamii na Utamaduni, Chuo Kikuu cha Freie Berlin) na Lutz Diegner (Mhadhiri wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Humboldt Berlin)
Katika Baraza letu la kwanza kupitia mtandao wa Zoom, wazungumzaji wanne kati ya watano walioalikwa watokao katika miji mikubwa minne walijadili maono yao juu ya tauni ya Korona na mabadiliko walioyaona katika jamii zao na maisha yao binafsi. Kwa sababu isiyoweza kuzilika, mzungumzaji wetu mahili Bwana Abdilatif Abdalla (Mwandishi wa “Sauti ya Dhiki”, Oxford University Press 1973) hakuweza kuhudhuria.
Akiongea kutoka Mombasa, Hassan Mwakimako alizungumza jinsi usitishwaji wa shughuli ulivyozuia matembezi ya watu katika kaunti za Kilifi, Mombasa na Kwale. Hii imepelekea kushindikana kwa kusafiri kwenda kazini kwa watumishi wanaoishi kwenye miji tofauti na wanayofanyia kazi. Mwanzoni, watu wengi walidhani kwamba ugonjwa huu ni wa ulaya tu. Hali ambayo imepelekea mgawanyiko kati ya wengi ambao waliudharau ugonjwa na wachache ambao waliamini ungonjwa huu upo. Hivyo baadhi ya watu hawakufuata sheria za kiafya dhidi ya ugonjwa huu kwa mgano kutokuvaa barakoa mpaka waone polisi. Toka hapo, mitaa ilipakwa rangi za ishara kuanzia zinazozuia mikusanyiko ya watu hadi kufungwa kwa misikiti. Hii imepelekea upunguaji wa shughuli za kichumi, upatikanaji wa mahitaji ya nyumbani kama samaki wa bahari, uhudhuriaji wa misiba (ukizingatia kizingiti cha watu 15) na kutembelea ndugu, jamaa na marafiki. Katika harakati za kutimiza hatua za kijikinga, neno la Kiswahili “barakoa” limefufuliwa na linatumika mara kwa mara. Katika nyanja za siasa, baadhi ya wanasiasa wameutumia ugonjwa kujijengea umaarufu kabla ya uchaguzi. Hii imekua kupitia jitihada zao kuwahamasisha watu kufuata kanuni zote za kiafya dhidi ya ugonjwa huu.
Kulingana na Nandera Mhando, Tanzania imedhibiti Korona tofauti. Kukiwa na maambukizi 480, waliopona 167 na vifo 16, serikali ya Tanzania iliamua kutangaza watu wanaopona na wale walioko mahospitalini. Pamoja na kuushauri umma kufuta kanuni za usafi dhidi ya Korona, serikali ya Tanzania haikuzuia watu kutoka nje. Wakuu wa serikali ambao ni rais, waziri mkuu na waziri wa afya walikazania hatua za kiafya. Rais na waziri mkuu walitilia mkazo kusali na kujifukiza kama njia kuu za kuepuka ugonjwa ambayo ilipokelewa na watu wengi nchi nzima. Hii iliamsha vipingamizi kutoka kwa wasomi ambao walidhani kuzuia watu kutoka nje kulikua sahihi. Kufikia tarehe 29 Aprili miji mikubwa ilijaa hofu za juu ya kuambukizwa ugonjwa huu. Kwa upande mwingine, vijiji na miji midogo haikuhofu kwa sababu shghuli zao za kila siku haziwaleti kwenye misongamano ya watu wengi. Hali iliyo pelekea kuaminika kwamba ugonjwa huu ni wa miji mikubwa tu.
Uwezo pungufu wa kupima na uhaba wa vifaa vya kujikinga, ulichangia uzinduzi kati ya wasomi na wajasiriamali. Chuo kikuu cha Dar es Salaam kilifanya utafiti uliopelekea kutengeneza barakoa na sanitaiza stahiki. Hii imechagiza utafiti juu ya uwezekano wa dawa za kienyeji zinazotibu Korona ndani ya chuo kikuu, Taasisi ya Utafiti wa Dawa na Taasisi ya Viwanda Vidogo Vidogo. Vilevile, imechangia utafiti juu ya tabia za watu katika kufuata sheria za kiafya dhidi ya ugonjwa wa Korona.
Kwa sababu ya uwezo pungufu wa kupima, watu katika miji mikubwa imewabidi waishi kwa uvumi mwingi kwa sababu hakuna takwimu sahihi juu ya maambukizi – na wamejifunza kuishi na ugonjwa. Kumwekua pia na kikomo cha wahudhuriaji kumi katika mazishi, ambayo imeathiri tamaduni ya ndugu kukutana pamoja na kuzungumza mambo ya kifamilia misibani. Hali ambayo imepelekea usambaaji wa picha za WhatsApp juu ya mazishi ya usiku wa manane na kuongezeka kwa makaburi katika miji mikubwa. Hofu iliongezeka. Baada ya serikali kuruhusu safari za misiba nje ya miji mikubwa, usambaaji wa picha hizi ulianza kupungua. Katika mwezi wa sita, utalii, mahoteli na shule zilifunguliwa – na wakati huo huo maandalizi ya uchaguzi yalianza. Yote kwa yote uvumi unaendela kusambaa na kufanya maisha yawe ya wasi wasi.
Akiongea kutoka New York, Nocholas Githuku alieleza kwamba mafunzo yamekua ya mtandaoni toka watu walipozuiwa kutoka nje – ambayo imewasumbua watu wazima maana hawajui kutumia teknolojia hii sana. Kama ilivyo Tanzania, kumekua na hofu sana za kuambukizwa pale watu wakitoka nje kufanya manunuzi ya muhimu. Kizuizi cha kutoka nje chini ya uongozi wa gavan Cuomo kumepelekea watu kukosa mazoezi. Hali iliyopelekea wao kufanya maamuzi binafsi. Kwa mfano, Nicholas Githuku alikimbia maili 80 katika mwezi wa Juni. Changamoto mbili za muhimu alizotaja ni kwamba imekua ngumu kutambua watu wa karibu kwa sababu ya barakoa. Alieleza wasiwasi kwamba kuweka umbali kunaweza kutumiwa kama kisingizio na watu ambao ni wabaguzi wa kitamaduni kwa ajili ya kubagua watu dhidi ya rangi ya ngozi. Hii inafuatia baada ya unyama wa askari wa Marekani ulipeleka mauaji ya George Floyd.
Neema Kasabo, mkazi wa Berlin kutoka Tanzania, alielezea kwamba kumekua na uhaba wa chakula katika masoko makubwa, matamasha na mikusanyiko ya waimba kwaya ilisitishwa na shule zilifungwa. Kwa kipindi fulani wazee hawakuweza kuwaona wajukuu zao ana kwa ana. Baadhi ya hoteli zilifunguliwa kwa ajili ya kuwajali watu wasio na makazi na baadhi ya watu waliwapatia chakula.
Kufuatia wazungumzaji, wahudhuriaji walichangia kwa uhai katika mazungumzo wakiuliza maswali na kuchangia katika mada. Maswali yalihusu changamoto za usawia wa kazi, kusimamia watoto kujifunzia kutoka nyumbani, kuzoea masomo ya mtandaoni na kufanya biashara. Mada mashuhuri ilichangiwa na mwanafunzi wa kike kutoka Cape Town ambapo mpaka baraza, ilikua ni siku ya 100 ya kutokutoka nje. Alieleza kua imepelekea changamoto za kiakili kwa mabinti ambao wamekua wakinyanyaswa kijinsia na vijana wa kiume wenye malengo mabaya ambao kwa sasa wapo nao mabwenini ukilinganisha na muda mchache kipindi walipokua wakienda shule.
Unaweza kupata habari zifananazo katika ukurasa wetu wa Korona. Mfano hali ya Maisha Mji wa kale, Mombasa, safari ya Abdilatif Abdallah Afrika Mashariki na mapokeo ya Uganda.
Deutsche Übersetzung
Hassan Mwakimako (Associate Professor of Religious Studies, Pwani University Kilifi, Kenya), Nandera Mhando (Head of Department, Philosophy and Religious Studies, University of Dar es Salaam), Nicholas Githuku (Assistant Professor of History, Philosophy and Anthropology, York College, CUNY, New York) und Neema Kasabo (Dozentin Suaheli-Kurse, Freie Universität, Berlin).
Einleitung und Begrüssung von den Gastgebern, Kai Kresse (Vizedirektor ZMO) und Lutz Diegner (Lektor für Swahili, Humboldt Universität Berlin).
In unserer ersten digitalen Diskussionsrunde über Zoom schilderten vier Sprecher aus vier verschiedenen Standorten ihre Erfahrungen in Zeiten der Coronavirus Pandemie und sprachen von Veränderungen, die sie sowohl in der Öffentlichkeit als auch in ihrem privaten Umfeld wahrgenommen haben. Einer unserer Sprecher, Abdilatif Abdalla (Autor von „Sauti ya Dhiki“, Oxford University Press 1973) konnte nicht anwesend sein.
Hassan Mwakimako (Mombasa) sprach von seinen Erfahrungen mit dem Lockdown in Kenia, infolgedessen das Reisen zwischen den Kilifi, Mombassa und Kwale Bezirken eingeschränkt wurde. Straßenschilder weisen darauf hin, große Gruppen zu vermeiden, zum Beispiel in Moscheen. Wirtschaftliche Aktivitäten, Zugang zu lokalen Waren und soziale Angelegenheiten wie Beerdigungen wurden dadurch deutlich eingeschränkt. Diese Maßnahmen bringen ein neues Wort im Suaheli zum Vorschein – „barakoa“, die Maske.
Nandera Mhando (Dar es Salaam) berichtete von den Maßnahmen der Regierung Tansanias, die hygienische Maßnahmen sowie zu Gott beten empfehlen. Zudem sprach Mhando davon, wie das Eindämmen des Virus hauptsächlich eine Sorge der Großstädte geworden ist.
Niedrige Testkapazitäten und ein Mangel an Schutzkleidung gaben Unternehmern den notwendigen Ansporn. Die Universität von Dar es Salaam führte Forschung durch und produzierte Masken und Desinfektionsmittel. Infolgedessen wurde die Erfindung von traditioneller Medizin gegen das Virus ermutigt, durch Forschung der Universität, dem National Institute for Medical Research und der Small Industries Development Organisation. Andererseits, aufgrund der niedrigen Testkapazität vertrauen Bewohner der Städte Gerüchten, da genaue Daten zu dem Verbreiten des Virus nicht existieren.
Nicholas Githuku (New York) wies darauf hin, dass aufgrund des Lockdowns ausschließlich digital unterrichtet wird. Zwei Herausforderungen sind die Identifikation von Menschen, die Masken tragen, und das Social Distancing als Ausrede für Diskriminierung gegen people of color verwendet wird, vor allem nach aktuellen Vorfällen der Polizeigewalt.
Neema Kasabo (Berlin) erzählte von Knappheit von Lebensmitteln in Supermärkten, Schulschließungen und abgesagten Konzerten und Chortreffen. Außerdem berichtete sie, dass Großeltern in dieser Zeit ihre Enkelkinder nicht persönlich treffen konnten und wie obdachlosen Menschen geholfen wurde.
Im Anschluss gab es eine lebendige Diskussion mit aktiver Beteiligung und kritischen Nachfragen. Zudem berichtete ein Mitglied des Publikums von Sorgen um die mentale Gesundheit weiblicher Studenten in Südafrika, die einerseits unter der Isolierung durch den Lockdown, und andererseits auch unter Belästigungen von Männern zu leiden haben.
Weitere Beiträge zu diesem Thema können Sie in unserem Corona Dossier finden. Zum Beispiel wird dort aus der Altstadt von Mombasa berichtet, Abdilatif Abdallah berichtet von einer Reise durch Ostafrika und es gibt einen Bericht über den Umgang Ugandas mit der Pandemie.